January 11, 2009

BALOZI MPYA WA UK BONGO

Serikali ya Uingereza, imemteua Diane Corner,kuwa Balozi wake mpya nchini Tanzania. Corner, anachukua nafasi ya Balozi Philip Parham aliyemaliza muda wake. Katika taarifa ya ubalozi huo iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana, ilisema Corner ataanza rasmi kazi ya ubalozi Februari, mwaka huu. Taarifa hiyo ilisema, Parham ambaye alikuwa balozi nchini kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, amethibitishwa kuwa naibu mwakilishi wa kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Parham alikuwa anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu. Aidha taarifa hiyo ilisema, kitaaluma, Corner, ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu mkubwa wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Aliwahi pia kuwa Kaimu Balozi nchini Zimbabwe. Taarifa hiyo ilisema Corner ameolewa na ana watoto wanne.

No comments: