September 22, 2022

October 26, 2019

Mwanamke wa Kenya aliyepotea Amepatikana amekufa huko Potsdam


Kijana wa Kenya, Britney kutoka Drewitz huko Brandenburg ambaye alikuwa amepotea Jumanne, amepatikana akiwa amekufa. Meya wa Potsdam ametoa pole kwa familia. Jumanne alasiri saa 3 usiku, mtu ambaye alikuwa amekwenda kuvua samaki kando ya mto wa Havel, aliita polisi akidai ameona mwili wa kike ukipanda kwenye maji. Mita chache kutoka ambapo mkoba wa Britney na mali zake binafsi zilipatikana Jumatano asubuhi na ambapo polisi na walinzi wa pwani walitafuta siku mbili.
Kufikia wakati Brigade ya Moto ilifika eneo la tukio, mwili ulikuwa umeshikwa na bollard na waliweza kuuweka kwenye mashua. Daktari wa dharura aliitwa na aliweza tu kudhibitisha kifo hicho. na kuwa mwili ni wa Britney. "Msichana bado alikuwa amevaa nguo ambazo aliripotiwa kuwa alikuwa amevaa, shati jeusi na shati jeupe, na bado alikuwa na simu yake ya mkononi. Tiketi yake ya mwezi ya treni ilikuwa bado mifukoni mwake, "Reinhold Hüpkes - mratibu wa operesheni ya wanamaji.
aliwaambia waandishi wa habari baada ya operesheni ya uwokozi.
Baada ya kuona maiti hiyo, polisi walishuku kuwa Britney alikuwa amekufa ndani ya maji tangu Jumanne iliyopita wakati alipopotea. Polisi wa uhalifu wa Shirikisho wameanza na uchunguzi juu ya kifo hicho, kwa sasa hakuna mtu yoyote anayeshukiwa na kifo hicho, uthibitisho wa mwisho utatolewa  mara tu uchunguzi utakapo kamilika.
Meya wa Mji wa Potsdam, Mike Schubert alijibu kwa huzuni kubwa na masikitiko kuhusiana na  habari ya kifo cha Britney: "Sote hapa Potsdam tumesikitishwa na  kifo cha mwanafunzi huyo kijana. Ni mbaya na cha kusikitisha wakati msichana mdogo kati yetu anakufa bila kutarajia. Ni bahati mbaya kwamba tumaini letu la kumpata akiwa hai halikuwezekana.
Tunatoa salamu zetu za pole na kuomboleza na familia na marafiki zake.

October 09, 2019

Viongozi wapya wa UTU e.V

Viongozi wapya wa UTU e.V
kutoka kushoto Bi. Petrida Karch Katibu, Bi Vanessa Fölsen M/kiti, Bw.Malumbo Salim Malumbo  Makamu M/kiti
Bw. Mngoya Lukuta Mweka Hazina

October 05, 2019

Watanzania wa Ujerumani wafanya Uchaguzi

Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya mkutano mkuu wa kuchagua viongozi mjini Aschaffenburg nchini Ujerumani siku ya jumamosi tarehe 28.09.2019.
Katika uchaguzi huo watanzania wanaoishi nchini ujerumani walichagua viongozi wapya , nafasi ya M/kiti  alichaguliwa Bi Vanessa Fölsen kuchukua nafasi M/kiti Mstaafu Bwana Mfundo Peter Mfundo aliyejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuitumikia takribani miaka 9. hata hivyo kamati ilimpendekeza Bwana Mfundo achukue nafasi ya heshima kuwa mwanakamti , mshauri na mlezi wa UTU e.V na kiongozi  muandamizi katika shughuli za UTU e.V
Watanzania wanaoishi ujerumani pia walichagua viongozi wafuatao
M/kiti:  Bi.Vanessa Fölsen
Makamu M/kiti: Bw. Malumbo Salim Malumbo
Katibu: Bi Petrida Karch
Mtunza Pesa:Bw.Mngoya Lukuta

wanakamati waliochaguliwa

Bw. Mfundo Peter Mfundo
Bw.Ebrahim Makunja (aka. Kamanda Ras Makunja )
Bw. Sudi Mnette

September 29, 2017

MWILI WA MSANII MAREHEMU MOHAMEDI IDDI MTURUMA KUWASILI DAR JUMAMOSI 30-09-2017 USIKU KUTOKEA NCHINI SPAIN

Umoja wa Watanzania Ujerumani  ( UTU ) ukishirikiana na watanzania wanaoishi Ujerumani na Spain , unawajulisha  ndugu, jamaa, Marafiki , wapenzi , na watanzania wote Duniani kuwa mwili wa Msanii marehemu Mohamed Iddi Mturuma aka MUDDY utasafirishwa leo Ijumaa Tarehe 29.09.17 na utafika siku ya Jmosi tarehe 30.09.17 saa 8:30 Usiku ( Nane na nusu usiku ) kuamkia Jpili katika uwanja wa ndege JKN Dar, mazishi yatafanyika nyumbani kwa marehemu huko Mbezi ya kimara , na taratibu za mazishi mnaweza kupiga simu Nr.0653319069   au 0656210725 ili kupata taarifa za mazishi lini yatafanyika, mwili wa Marehemu utasindikizwa na rafiki wa karibu wa Marehemu Mussa Selemani aka Moses Fab anayeishi Uingereza .
Marehemu Muddy allikuwa anaishi nchini ujerumani na umauti ulimfika tarehe 28.09.17 nchini Spain ambako alikwenda kufanya shughuli zake za usanii wa sarakasi .

Allah amlaze mahala pema pepeoni 

Ameen 

June 08, 2015

Raisi wa Zanzibar Dr.Ali Mohammed Shein Azungumza na Watanzania waishio Ujerumani

Mhe. Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazi la Mapinduzi akiwa na Mwenyekiti wa UTU. Mfundo Peter Mfundo
Mhe. Balozi wa Tanzania Ujerumani Mh.Philip S. Marmo akimkaribisha Mhe.Raisi Dr. Shein kuongea na Watanzania
                                                        Mhe Raisi na Mwenyekiti wa UTU

 Mwenyekiti Wa UTU akiongea kwa Niaba ya Watanzania wa Ujerumani
Mhe. Raisi Dr. Shein na Watoto wa Kitanzania
 Malumbo´s Jr  na Naibu waziri mambo ya nje Mhe. Mahadhi
Mhe. Rais Dr. Shein katika Picha ya Pamoja na Watanzania wa Ujerumani

Watanzania nchini Ujerumani wamekumbushwa kujijenga nyumbani kwa shabaha ya kustawisha maendeleo ya nchi na maisaha yao kwa ujumla. Hayo yamesemwa na  Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein pale alipozungumza na watanzania waishio nchini ujerumani katika Mji wa Würzburg.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika sambamba na Tamasha la siku 4 la Kimataifa la 27 la muziki wa Afriaca ambalo kwa mwaka huu zingatio kubwa ilikuwa Zanzibar

March 30, 2015

ALI KIBA & JIDE WAFUNIKA DAR

 MwanamuzikiLady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
Tumefunika mbaya mtu wangu....ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.
Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22