July 04, 2009

Yemenia yasimamisha safari zake za ndege Comoro

Shirika la ndege la Yemen-YEMENIA, limetangaza kusimamisha safari zake za ndege kwenda Comoro, kufuatia ajali iliyotokea Jumanne iliyopita, karibu na mji mkuu wa Visiwa vya Comoro, Moroni.
Taarifa iliyotolewa na afisa wa shirika hilo la ndege imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kufuatia ajali za hivi karibuni na hatua ya abiria kuvamia viwanja vya ndege, na kwamba safari hizo zitarejea hali itakapokuwa shwari.
Mwanasheria wa shirika la ndege la Yemenia, Laurent-Franck Lienard nchini Ufaransa, amesema kuwa ndege zilizosimamisha safari zake ni zile za Moroni peke yake na kwamba ndege za shirika hilo zitaendelea na safari zake katika maeneo mengine kama kawaida.
Ndege hiyo chapa Airbus A 310, iliyokuwa na abiria 153, ilianguka katika Bahari ya Hindi nje ya pwani ya Visiwa vya Komoro na hadi sasa ni abiria mmoja tu ndiye amesalimika
.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22