Kiota cha maraha Belleville, Oslo, kitawaka moto mkali wakati Ras Nas na kikosi chake watakapofanya kweli Ijumaa tarehe 28 mwezi huu. Tumbuizo hili ni la kwanza mwaka huu kwa Ras Nas ambaye ameahidi kufanya shoo la kufa mtu. Safu ya wanamuziki safari hii inajumuisha mpiga sax mahiri toka Mozambique, Ivan Mazuze, mkaanga chipsi (drummer) Uriel Seri toka kwa Gbagbo, Ivory Coast, na mkun'guta besi Aristide Milongo tokea Congo Brazzaville. Wengine ni Dag Pierre, gitaa toka Sweden na Thor Erik mpiga kinanda toka Norway. Mwanamuziki Ras Nas ajulikanaye pia kwa jina halisi la Nasibu Mwanukuzi anachanganya mitindo ya reggae na muziki wa dansi. Kama upo Oslo usikose kujionea mwenyewe kwa macho yako. Usingoje kuambiwa!
Tarehe: Ijumaa 28 January
Mahali: Belleville, Cosmopolite (Vogstgate 64) Shoo: Kuanzia 22.00 hrs
Shoo: Kuanzia 22.00 hrs
No comments:
Post a Comment