September 07, 2011

Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge La Vijana London‏

Miss Jestina akifanya mahojiano
Picha ya pamoja na Naibu Balozi





Ubalozi wetu wa Tanzania Hapa Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde ili kwenda kutuwakilisha katika mkutano wa nne wa Commonwealth Youth Parliament ( Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10 Septemba 2011 jijini London. Mkutano huu Umeandaliwa na Commonwealth Parliamentary Association tawi la Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya CPA ambayo ni Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa kwanza kuteuliwa na Pia ni Mtanzania mwenzetu Dr William Shija.
Lengo kuu la mkutano huu ni kuwawezesha vijana kati ya miaka 19-29 kwa kuwapatia uzoefu wa shughuli za Bunge hasa katika kuimarisha demokrasia ya mabunge na Uchumi. Motto wa Mkutano wa mwaka huu "MABADILIKO YA HALI YA HEWA"
Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza unapenda kuwapongeza sana Linda Kapinga na Lucy Minde kwa kuchaguliwa kwao na pia kuwatakia kila la kheri katika kutuwakilisha kwenye mkutano huu.
Asanteni,
Urban Pulse ikishirikiana Miss Jestina Blog Na Ubalozi wa Tanzania

1 comment:

Ran Midou said...

hmmmmm..-_-;
visit my blog eh?
http://blogkerenane.blogspot.com/2011/09/monk-who-mummified-himself-till-he-died.html

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22