February 10, 2012

Ahukumiwa maisha gerezani

Mwanaume mmoja mzaliwa wa Kosovo alihukumiwa na mahakama moja ya Ujerumani leo kifungo cha maisha gerezani kwa mauaji ya mwaka jana ya wanajeshi wawili wa Marekani katika uwanja wa ndege wa Frankfurt. Arid Uka pia alihukumiwa kwa mashtaka matatu ya kujaribu kuuwa. Mshukiwa huyo, mwenye umri wa miaka 22 alikuwa ndani ya basi lililokuwa na wanajeshi hao wawili wa Marekani katika uwanja wa ndege wa Frankfurt mwezi Machi na akaanza kuwafyatulia risasi. Alizuiwa tu kuendelea kuwauwa watu zaidi wakati bastola yake ilipokwama na akazidiwa nguvu na wanajeshi waliokuweno ndani ya basi hilo. Shambulio hilo limetajwa kuwa la kwanza kufaulu nchini Ujerumani lenye kuchochewa na waislamu wenye siasa kali, ijapokuwa wapelelezi walisema hakuna ushahidi kuwa Uka alikuwa na uhusiano na kundi lolote la kigaidi.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22