Na Mwandishi Wetu
BENDI Kongwe ya Msondo ngoma ya jijini Dar es salaam inatalajia
kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya kabisa wa kisasa wa burudani wa
Emirate Hall uliopo Masasi June 2 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa bendi hiyo Rajabu
Mhamila 'Super D' Alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku
ya ufunguzi wa ukumbi huo ambapo watatoa burudani isiyo na kifani
;unajua sisi ni baba ya Muziki nchini ndio mana wapenzi wengi
wanaitaji burudani kutoka kwetu ndio mana tunapopata nafasi ya kwenda
mikoani tunakwenda kama hivi tumealikwa kutoa burudani siku hiyo
tutatoa burudani ya uhakika
siku hiyo tutapiga vibao vetu vya zamani na vipya kwa sasa alivitaja
baadhi ya vibao vitakavyonogesha uzinduzi huo kuwa ni Suluhu wa
Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa
Eddo Sanga hizo ni baadhi ya nyimbo mpya zitakazonogesha siku hiyo
vile vile watapiga nyimbo zao za zamani
zilizotamba wakati huo Alisema Super D Kundi hilo litaambatana na
wanamziki wake wote wakiwemo wakongwe katika mziki wa Dansi Nchini
Maalimu Gulumo ' Kamana' Saidi Mabela ' DKT Mabela' na wengine wote
watafanya vitu vyao siku hiyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki
wao wa Masasi Aliongeza Super D
No comments:
Post a Comment