July 18, 2008

German Chancellor Merkel Promotes Business Ties With Algeria

The mosque's tower will become a new landmark in Algiers

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Abdelaziz Bouteflika katika siku ya pili ya ziara yake nchini Algeria.
Kansela Merkel ameweka mkazo katika masuala ya biashara kwenye ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kwake kuifanya katika eneo la Kaskazini mwa Afrika.
Algeria ni nchi ya tatu kwa kusambaza gesi barani Ulaya, ambapo Kansela Merkel amesema kuwa anataka kuanzisha ushirikiano na Algeria katika nishati hiyo ya gesi ili kukidhi mahitaji ya gesi nchini Ujerumani.
Aidha Kansela Merkel alitoa wito wa kuimarishwa kwa haki za wanawake katika nchi hiyo ya kiislam.
Kufutia ziara hiyo kampuni moja la kijerumani limefanikiwa kupata kandarasi ya ujenzi wa msikiti mjini Algears utakaokuwa wa tatu kwa ukubwa duniani ujenzi ambao gharama yake ni kiasi cha euro billioni moja.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22