March 30, 2015

ALI KIBA & JIDE WAFUNIKA DAR

 MwanamuzikiLady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
Tumefunika mbaya mtu wangu....ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.
Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.

OMMY DIMPOZ LIVE IN ZURICH


Uchaguzi Nigeria; wananchi watakiwa kuwa watulivu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipongeza Nigeria kwa kuendesha uchaguzi kwa kiasi kikubwa kwa amani na utaratibu mzuri.
Lakini Ban amewataka wananchi kuendeleza hali ya amani na kuwa na subira, na ameshutumu mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Waislamu la Boko Haram pamoja na makundi mengine ya wanamgambo waliojaribu kuchafua uchaguzi huo wa rais na bunge. Zoezi la kuhesabu kura linaanza rasmi mchana huu, na matokeo yanatarajiwa baadaye leo Jumatatu.
Muda wa kupiga kura waongezwa
Upigaji kura ulilazimika kufanyika kwa siku mbili bila kutarajiwa na baadhi ya majimbo ya kupigia kura yalifanya hivyo jana Jumapili baada ya matatizo kutokea katika matumizi ya teknolojia mpya yenye utata ya kuwatambua wapiga kura na mara nyingine hata wasimamizi wa vituo vya kupigia kura hawakufika mahali wanapotakiwa kusimamia kama mkaazi huyu alivyolalamika.
"Lalamiko langu ni kwamba tuko hapa tangu Jumamosi. Hatujamuona afisa wa tume jana,maafisa wengine hawakuja na hatuelewi kuna nini. Tunasubiri. Watu wako hapa tangu tulipotarajia kupiga kura, watu wamejitokeza tangu alfajiri".
Lakini mkuu wa tume ya taifa ya uchaguzi Attahiru Jega amesema tume yake ina imani kwamba lengo lake la kufanya uchaguzi ambao ni huru, wa haki , wenye kuaminika na wa amani linaelekea kutimia. Afisa wa tume hiyo Amina Zakari anathibitisha hilo.
"Hali iliyopo sasa ni kwamba uchaguzi ulifanyika kwa mafanikio katika maeneo mengi, lakini huwezi kutarajia uwe bila matatizo katika maeneo yote".
Matatizo ya kiufundi
Matatizo ya kiufundi katika zoezi la kupiga kura , hata hivyo , yalianzisha hamasa zinazoelekeza kuwa na uwezekano wa mzozo wakati chama cha rais Goodluck Jonathan cha PDP kupinga matumizi ya chombo hicho cha kutambua wapiga kura , kikisema vifaa hivyo havikufanyiwa majaribio ya kutosha.
Chama cha Buhari cha All Progressives Congress APC kinaunga mkono mfumo huo mpya kama seemu ya kuzuwia udanganyifu katika upigaji kura ambao umechafua chaguzi zilizopita.
Kundi la asasi za kijamii nchini Nigeria linaloangalia uchaguzi huo limeonya leo Jumatatu kuhusu udanganyifu katika uchaguzi huo , likisema linawasi wasi mkubwa kutokana na ripoti za majaribio katika majimbo kadhaa nchini humo kuvuruga zoezi la ukusanyaji wa matokeo jumla ya uchaguzi huo.

Chanzo. DW.


June 08, 2014

Malumbo´s Junior kurudi Hewani hivi Karibuni

Hallow Wadau wa Malumbo´s Junior
Samahani kwa Usumbufu Uliojitokeza tangu Januari.
Kutokana na matatizo ya kiufundi ambayo kwa sasa yamesharekebishwa Blog yenu itarudi Hewani hivi Karibuni


Akhsanten

Malumbo´s Jr.

January 05, 2014

RAIS KIKWETE NA MAKAMU DKT. BILAL WAWAONGOZA WANANCHI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. MGIMWA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko
Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho.

January 04, 2014

Mazungumzo ya amani Sudan Kusini bado kitendawili

Wapatanishi wamesema kuwa sasa haijulikani wazi kama waasi wa Sudan Kusini wataanzisha mazungumzo ya ana kwa ana na serikali, hali ambayo imeondoa matumaini ya kusitishwa mapigano mara moja ili kuiepusha nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. 
Mazungumzo yaliyopangwa katika nchi jirani ya Ethiopia,  tayari yamecheleweshwa mara kadhaa, pamoja na kuwa na mwanzo mbaya. Pande zote mbili walikutana na wapatanishi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi IGAD kwa siku ya pili hii leo lakini hawakukaa katika meza moja.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Ethiopia Dina Mufti amesema bado wanaendelea kutayarisha agenda kuu  ya mazungumzo hayo ambayo itakubaliwa na pande zote.  
Mapigano yalizuka mwezi uliopita katika nchi hiyo changa kabisa ulimwenguni, baada ya Rais Salva Kiir  kumtuhumu aliyekuwa naibu wake kwa kupanga jaribio la mapinduzi ambalo halikufaulu. 
Maelfu wanahofiwa kuuwawa na wengine 200,000 wameyakimbia makaazi yao.

Chanzo. Dw.

HAPPY NEW YEAR

NAWATAKIA WADAU WOTE HERI YA MWAKA MPYA

September 03, 2013

AFRICAN PARTY KÖLN

HAYA TENA WADAU WA KÖLN NA VITONGOJI VYAKE 
ULE WAKATI MLIOKUWA MNAUSUBIRI NDIO SASA UNAWADIA 
NA SIKU ZINAANZA KUKATIKA
DJ RAMA NA KIKOSI CHAKE  KIZIMA KUTOKA MUNICH WANATARAJIWA KUWASHA MOTO KATIKA JIJI LA KÖLN
DJ  RAMA ANAKULETEA NGOMA ZOTE MPYA KUTOKA EAST AFRICA.
BONGO FLAVA, MDUARA, KWAITO, AZONTO, 

SIKU YA  IJUMAA  TAREHE  06.09.13
KUANZIA SAA 3:00 USIKU (21:00 HRS)

Diamond Platnumz - Number One Behind the scene

August 24, 2013

LULU ATINGA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU KWA AJILI YA FOOLISH AGE

 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi.
 Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”.
Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi.

KAMPUNI ya Proin Promotions imewasilisha filamu yake iliyopewa jina la “Foolish Age” kwa Bodi ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukaguzi ambapo baada ya kufanyiwa marekebisho filamu hiyo inaweza kuruhusiwa katika uzinduzi wa Kampuni hiyo hivi karibuni.
Bodi ilifikia hatua ya kuwaita wahusika yaani Proin Promotions na Elizabeth Michael (Lulu) kwa ajili ya kufanya majadiliano kuhusu maudhui na maadili katika filamu hiyo kabla ya kufanyia maamuzi.
Katika majadiliano hayo Bodi ya Filamu iliwakumbusha wahusika hao kufanya baadhi ya marekebisho katika filamu hiyo ili iweze kuwa kivutio kwa umma, pia Bodi ya Filamu iliwakumbusha juu ya umuhimu wa kuzingatia kifungu cha 14 cha Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ambacho kinaipa Bodi mamlaka ya kukagua filamu, matangazo na maelezo yote na kile cha 24 (1) (d, n na t) cha Kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kinachofafanua mambo yanayotakiwa na yale yasiyotakiwa katika filamu ambayo filamu hiyo imekwenda kinyume.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Bi. Gift Msuya alikubaliana na ushauri uliotolewa na Bodi ya Filamu na aliiomba Bodi itoe muda kwao kwa ajili ya kufanyia marekebisho katika filamu hiyo.
Naye msanii Elizabeth Michael (Lulu) aliieleza Bodi ya Filamu kuwa Filamu hiyo aliitengeneza muda mrefu na kwa sasa atazingatia maelekezo ya sheria, Kanuni na taratibu hususani katika eneo la maadili. Aidha alikiri kuwa ni kweli maeneo yaliyobainishwa kweli yanahitaji marekebisho.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Fissoo alimalizia kwa kuishauri Kampuni hiyo kutotumia filamu hiyo katika uzinduzi wa kampuni yao hadi hapo watakapofanyia marekebisho katika baadhi ya maeneo muhimu ndani ya filamu hiyo.

Proin Promotions ni Kampuni inayojikita katika kuandaa na kutengeneza filamu za kitanzania na kuzisambaza nchini, pia ni kampuni inayotarajiwa kutoa ushindani mkubwa katika tasnia ya filamu. Kampuni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya maandalizi rasmi kukamilika.

Source: Teamtz.