Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya mkutano mkuu wa kuchagua viongozi mjini Aschaffenburg nchini Ujerumani siku ya jumamosi tarehe 28.09.2019.
Katika uchaguzi huo watanzania wanaoishi nchini ujerumani walichagua viongozi wapya , nafasi ya M/kiti alichaguliwa Bi Vanessa Fölsen kuchukua nafasi M/kiti Mstaafu Bwana Mfundo Peter Mfundo aliyejiuzulu nafasi hiyo baada ya kuitumikia takribani miaka 9. hata hivyo kamati ilimpendekeza Bwana Mfundo achukue nafasi ya heshima kuwa mwanakamti , mshauri na mlezi wa UTU e.V na kiongozi muandamizi katika shughuli za UTU e.V
Watanzania wanaoishi ujerumani pia walichagua viongozi wafuatao
M/kiti: Bi.Vanessa Fölsen
Makamu M/kiti: Bw. Malumbo Salim Malumbo
Katibu: Bi Petrida Karch
Mtunza Pesa:Bw.Mngoya Lukuta
wanakamati waliochaguliwa
Bw. Mfundo Peter Mfundo
Bw.Ebrahim Makunja (aka. Kamanda Ras Makunja )
Bw. Sudi Mnette
No comments:
Post a Comment