September 29, 2017

MWILI WA MSANII MAREHEMU MOHAMEDI IDDI MTURUMA KUWASILI DAR JUMAMOSI 30-09-2017 USIKU KUTOKEA NCHINI SPAIN

Umoja wa Watanzania Ujerumani  ( UTU ) ukishirikiana na watanzania wanaoishi Ujerumani na Spain , unawajulisha  ndugu, jamaa, Marafiki , wapenzi , na watanzania wote Duniani kuwa mwili wa Msanii marehemu Mohamed Iddi Mturuma aka MUDDY utasafirishwa leo Ijumaa Tarehe 29.09.17 na utafika siku ya Jmosi tarehe 30.09.17 saa 8:30 Usiku ( Nane na nusu usiku ) kuamkia Jpili katika uwanja wa ndege JKN Dar, mazishi yatafanyika nyumbani kwa marehemu huko Mbezi ya kimara , na taratibu za mazishi mnaweza kupiga simu Nr.0653319069   au 0656210725 ili kupata taarifa za mazishi lini yatafanyika, mwili wa Marehemu utasindikizwa na rafiki wa karibu wa Marehemu Mussa Selemani aka Moses Fab anayeishi Uingereza .
Marehemu Muddy allikuwa anaishi nchini ujerumani na umauti ulimfika tarehe 28.09.17 nchini Spain ambako alikwenda kufanya shughuli zake za usanii wa sarakasi .

Allah amlaze mahala pema pepeoni 

Ameen 

No comments: