July 09, 2008

ZAMBIA YAKANUSHA KIFO CHA RAISI WA NCHI HIYO

Waziri wa habari na huduma ya matangazo wa Zambia Bw. Mike Mulongoti tarehe 3 Julai ametoa hotuba kupitia televisheni akikanusha habari kuhusu rais Levy Patrick Mwanawasa wa nchi hiyo amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kiharusi huko Paris.
Bw. Mulongoti amesema, hivi sasa rais Mwanawasa bado anatibiwa huko Paris, na habari kuhusu amefariki dunia ni uwongo mtupu.
Awali radio ya Afrika ya Kusini imeripoti kuwa, Rais Levy Patrick Mwanawasa wa Zambia aliyelazwa hospitali wiki iliyopita amefariki dunia huko Paris, lakini habari hiyo imekanushwa mara moja na waziri wa mambo ya nje wa Zambia Bw. Kabinga Pande.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22