Mazingira yenye utata kuhusiana na kuawa kwa mwanamke wa Kimisri kwa kuchomwa visu hapa Ujerumani, yanajadiliwa na wakuu wa Ujerumani na Misri.
Msemaji wa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel , amesema kuwa Kansela huyo anatarajiwa kukutana na Rais Hosni Mubarak wa Misri pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa G8 huko Italia, hapo kesho.
Tukio hilo la kuchomwa visu mwanamke huyo wa Misri hapa Ujerumani limeamsha hasira nchini Misri. Serikali ya Ujerumani imekuwa ikilaumiwa vikali kwa kushindwa kuchukua hatua mujarab kuhusiana na tukio hilo, ambapo mwanamke huyo aliyekuwa mjamzito aliuawa katika ukumbi wa mahakama na mwanamme mmoja wa kirusi, anayetuhumiwa kumfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi katika uwanja wa michezo.
No comments:
Post a Comment