October 20, 2009

SHINDANO LA UNIQ MODO


  • Shindano la Uniqmodo limetokana na kawaida ya kutoa kiasi cha shillingi kati ya 50/100,00/= kwa mwezi kwa mamodo ambao kwa ridhaa yao, hutuma picha na maelezo yao kwenye blog yangu ili niwakuze miongoni mwa wadau wa maswala ya umodo. Ni faraja kuona kwamba wengi sasa wanapata kazi za umodo.
  • Blog ya Umodo inakaribia kutimiza mwaka mmoja, nikaona ni vema niitishe shindano kubwa zaidi litakaloshirikisha mamodo wa kike kwa mwaka huu ili nitoe zawadi ya jumla ya miezi 12. Yaani 1,200.000/=.
Hilo lilikuwa wazo langu hadi ambapo nilipojiunga na Gazeti jipya liitwalo Ok! Kila Wiki. Dau likaongezeka.
Mfumo wa shindano nao ukabadilika, na sasa tutafanya usaili wa wasichana wengi iwezekanavyo kutoka wilaya 3 za Dar es salaam.

Usaili utaanza tarehe 7 Novemba na tutachuja wasichana hadi wafikie 20 kila Wilaya na ndio hao watakaowakilisha wilaya.
Kigezo kikuu ni: UZURI HALISIA. Yaani NATURAL BEAUTY. Hatutajali sana ufupi, urefu, nk. Hii inatokana na "aina" ya wasichana waliopo nchini na pia Umodo kama unavyofahamu sio kupita jukwaani tu.

Kuelekea mwisho wa Mwezi Oktoba, naweza kuomba msaada wako zaidi na hata ushiriki ukiwa ni mdau mkuu wa maswala ya UREMBO.
Kwa leo, naomba hisani yako ya kubandika tangazo hili na maelezo ambata kwenye blog yako.

Nipo tayari kwa ushauri na kujibu maswali zaidi. Nitashukuru ukimwambia na rafiki mwingine.

Natanguliza shukrani!

Taji Liundi
Mmiliki Mwwendeshaji wa modotz.blogspot.com

No comments: