August 21, 2010

NGOMA AFRIKA LIVE IN HAMBURG

kamanda Ras Makunja


Muziki wa Ngoma Africa Band wapokelewa kwa NGUVU na KASI Kubwa Zaidi na washabiki
FFU wa Ngoma Africa Band wakitingisha jukwaa la World Music Festival,Mjini Loshasen,ujerumani ambapo muziki wao ulikubalika na washabiki na kuweka rekodi ya kuwa bendi bora iliyoweza kuwanasa washabiki na kupelekana puta bila mapunziko.
Bendi hiyo yenye tabia za kuwadatisha akili washabiki na mdundo wao wa "Bongo Dansi" imejizolea umaarufu kila kona ya duniani na kufanikiwa kujizolea mialiko ya kutumbuiza katika majukwaa mbali mbali,
kutokana na tabia zao hizo za kuwadatisha Akili washabiki kwa njia ya muziki "Ngoma Africa band" imejikuta bize bila ya kumpuzika kwa kuwatumikia washabiki na kuwapa muziki ambao unahitajika kwao!
hata hivyo gwaride la FFU litaendelea kupiga kasi kwa nguvu katika jukwaa la ALAFIA Festival mjini Hamburg,ujerumani siku ya 29.08.2010
onyesho litafanyika katikati ya kitovu cha mji wa Hamburg,Hamburg-Altona.

Pata raha zaidi at www.myspace.com/thengomaafrica

No comments: