September 10, 2011

TEMEKE KINONDONI NANI ZAIDI KATIKA MASUMBWI‏

MABONDIA Mbwana Matumla wa Temeke na Francis Miyeyusho wa Kinondoni Dar es Salaam wanatarajia kupanda ulingoni katika pambano la kudhihirishiana ubabe kati ya mabondia wa Temeke na Kinondoni litakalofanyika Oktoba 30 mwaka huu.

Pambano hilo pia litafuatiwa na lingine kati ya Ramadhani Shauri wa Kinondoni dhidi ya Issa Sewe wa Temeke ambapo yote yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Msaidizi wa Kambi ya Kinyogoli Foundation ya Dar es Salaam, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema mapambano hayo yameandaliwa na Promota Mohamedi Bawaziri kuhamashisha mchezo huo.

"Mabondia wote wameanza mazoezi na kwa upande wa Temeke wapo kambini chini ya Kinyogori Foundation chini ya kocha Habibu Kinyogori akishirikiana na mimi na tunawaandaa kucheza ngumi za kisasa sio kurusha ngumi bila mpangilio.," alitamba Super D

Alisema pambano kati ya Matumla na Miyeyusho litakuwa la uzani wa Bantam Weight kilogramu 54 ambapo Shauri na Sewe watacheza kilogramu 58, uzito mwepesi (Light Weight).

Alisema licha ya kuhamasisha, kumekuwepo na tambo za mda mrefu kati ya mabondia wa Kinondoni, na wenzao wa Temeke ambapo mashabiki watajionea mapambano hayo.

Kocha huyo alisema mapambano hayo yatasindikizwa na mengine kutoka kwa mabondia wa Temeke na Kinondoni ambapo pia kutakuwepo na burudani mbalimbali zitakazotangazwa baadae.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22