Napenda kutoa shukurani zangu za pekee kwa Mwenyezi Mungu, Familia yangu, Marafiki zangu, mashabiki wangu, wadau na watanzania wote kwa ujumla walioweza kunipigia kura ambazo zimefanikisha blog yaMissJestinaGeorge kuibuka kidedea na kunyakua ushindi mkubwa wa kuwa ''BLOG BORA YA MWAKA 2011'' katika tuzo za BEFFTA zilizofanyika nchini UK mapema wiki iliyopita.
Mchakato mzima wa kumtafuta mshindi ulikuwa na changamoto lukuki ukizingatia ya kwamba kulikuwa na jumla ya blogs 15 za kimataifa kutoka nchi mbali mbali Duniani. Kutokana na ushirikiano wenu mzuri mmeiwezesha blogu yetu kupata ushindi mnono na vile vile kunipatia fursa nzuri ya kuiwakilisha vyema Tanzania Ughaibuni.
Ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja kwa mchango wenu uliosadia kuwezesha blog yetu kunyakua ushindi mkubwa ingawa ningependa kuwatambua wafuatao: kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu zote za dhati kwa timu ya URBAN PULSE CREATIVE kwa mchango wao mkubwa waliotoa, wanachama wenzangu wa AMTTA (Amka Mwanamke Twende Tujikomboe Afrika) kwa kuwa na mimi bega kwa bega nawapenda sana. Pia natoa shukrani kwa Bloggers wenzangu wote, tovuti mbalimbali, TONE RADIO popote pale walipo kwa michango yenu.
No comments:
Post a Comment