MAISHA SAMSON
bondia wa ngumi za kulipwa kutoka kyela mkoani mbeya MAISHA SAMSON ameahidi kumtwanga mpinzani wake THOMAS MASHALI kwa knock-out ya raundi ya 9 ktk pambano lao litakalo fanyika tarehe 24-06-2012 katika ukumbi wa FRIENDs- CORNER ulioko jijini dar-es-salaam.
ktk pambano hilo la raundi 10 thomas mashali atakuwa anatetea ubingwa wake wa taifa unaotambuliwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini tanzania chini ya rais wake YASSIN ABDALLAH -USTAADH.
Mabondia hao watapigana ktk uzito wa kati [middle kilo 72.5 .maisha amesema anasikia sana sifa za mashali anayejiita SIMBA ASIYEFUGIKA,lkn ajuwe siku ya pambano atamuonesha kazi ngumu na akamtaka mashali awe mvumilivu ulingoni kwani yeye ni tofauti na ambao mashawahi kuwapiga.
nina mapambano 8 ambayo sijapigwa hata pambano moja na nimepigana na mabondia wajeuji zaidi ya THOMAS MASSHALI ,na wanatoka nchi za malawi ,zambia na namibia ,hivyo siona sababu kwa nini nishindwe kumpiga THOMAS MASHALI na kumpora mkanda wake na kurudi nao kyela [mbeya] alijigamba bondia huyo kutoka mkoani mbeya.
kwa kumalizia nawataka wazawa wa mkoa wa mbeya waishio dar-es-salaam wafike kwa wingi siku hiyo ya pambano kushuhudia kiyama nitakachomshushia THOAS MASHALI. Alimliza kusema maisha samsom.
mabondia wa ngumi za kulipwa tarehe 30-06-2012 ktk ukumbi wa community center watapambana na mabondia kutoka dar-es-salaam katika pambano lenye lengo la kumuenzi bondia magoma shabaani aliyfariki dunia hivi karibuni.promota wa pambano hilo ndg ally mwazoa amesema sehemu ya mapato hayo yataisaidia familia ya magoma shabani.
na hii ni ratiba ya kuendelea na siyo ya muda ,tutajitahidi kufanya hivyo kila baada ya miezi 6 kwani magoma ameacha familia ambayo ilikuwa inamtegemea hivyo ni wajibu wetu sisi familia ya ngumi za kulipwa tendelee kuwa pamoja na familia yake.
hivyo ninawataka wapenzi wa masumbwi na wapenzi wa magoma shabani kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwa ajili ya kufanikisha lengo la mapambano haya
mapambano haya yatasimamiwa na TPBO
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
No comments:
Post a Comment