April 20, 2008

BREKINK NYUUZZZZZZZZZ !!!!

Marehemu Ukiwaona Ditopile mzuzuri wakati wa Uhai wake

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bwana Ukiwaona Ditopile Mzuzuri amefariki dunia mjini Morogoro. Habari zinasema Bwana Ditopile ambaye alikwenda Morogoro juzi akitokea Tabora, alifariki dunia saa tatu leo asubuhi katika hoteli ya Hilux ya mjini humo. Mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Habari zaidi za kifo hicho tutawaletea katika taarifa zetu za habari zinazofuata.

No comments: