July 03, 2008

RAIS MWANAWASA AFARIKI DUNIA

Rais wa Zambia Levy Mwanawasa pichani amefariki mjini Paris nchini Ufaransa katika hospitali moja baada ya kuugua kiharusi ghafula mapema wiki hii.Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa ubalozi wa Zambia nchini Afrika Kusini.Maafisa nchini Zambia bado hawajasema lolote mpaka sasa.
Rais Mwanawasa aliye na umri wa miaka 59 alikimbizwa hospitali siku ya Jumapili alipokuwa mjini Sharm el Sheikh Misri baada ya kuugua kiharusi ghafla kabla ya kuhudhuria kikao cha Umoja wa Afrika.Alihamishwa mjini Paris,Ufaransa kwa matibabu baada ya hapo.
Bwana Mwanawasa alikuwa mwenyekiti wa Jumuia ya maendeleo ya mataifa ya kusini mwa Afrika SADC ambayo imekuwa msuluhishi mkuu katika mzozo wa kisiasa unaokumba nchi ya Zimbabwe.Kiongozi huyo aliugua kiharusi mwaka 2006 ila kabla ya kuchaguliwa tena mwaka huo alithibitisha kuwa afya yake iko salama.

1 comment:

heri said...

mpaka leo tarehe 4/7 habari hizi si za kweli. rais huyu bado yuko matibabuni na kwa mujibu wa taarifa za bbc swahili anaendelea vizuri na matibabu.

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22