Pablo na Vumbi
Maestro Vumbi
wadau wakilisakata sendema la nguvu
Siku ya jumamosi tarehe 09.08.08 nilipata bahati ya kukutana na mwanamuziki wa zamani wa maquis original ya mjini dar Alain Kahanga Dekula "Vumbi" ambaye kwasasa analiendeleza libeneke katika mji wa Stockholm.Vumbi na Pablo machine Wanatoa burudani kila siku ya ijumaa na jumamosi katka club moja ambayo ipo Stockholm Södra Centrum.
Mwanamuziki huyu alijulikana sana enzi hizo za maquis original kwa upigaji wake solo gitaa katika nyimbo kama vile makumbele, mayanga na nyingi nyinginezo.
Pia nilipata muda kidogo wa kuongea naye na kunipa historia fupi ya maisha yake tangu kuzaliwa kwake, maisha aliyopitia na mpaka hapa alipofika sasa.
Historia yake kwa kifupi.
Alain Kahanga Dekula "Vumbi" alizaliwa mji wa kivu katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambapo alisoma elimu ya msingi na Secondary, baada ya kumaliza Elimu yake ya Secondary katika mji wa Kivu (Uvira)alianza kujishughulisha na mambo ya muziki.
Alianza kupiga solo gitaa na bendi kama Bavy National, Grand mike jazz of Rashid king akishirikiana na wanamuziki kama Dr Remmy Ongala, baada ya hapo alihamia Dar es salaam ambako alifanya kazi na Maquis Original wana sendema moja ya bendi bora na maarufu Afrika mashariki na kati angalia "Worlds Music Rough Guide."
Maquis Original katika nyimbo zake kama vile ngalula na makumbele zilimshirikisha mpiga solo gitaa mwenye uwezo wa hali ya juu katika fani hiyo "Vumbi kahanga" kama anavyojulikana na wapenzi wengi wa muziki wa dansi kutokana na kulitumia kwa ufundi wake mkubwa gitaa la solo.
kwasasa anashirikiana pia mwanamuziki mashuhuri Pablo machine
unaweza kupata program yao kupitia
http://www.pablomachine.podomatic.com/
http://www.sokoafrica.net/
pia unaweza kuagizia cd yao mpya inayoitwa Sultan Qaboos

1 comment:
mambo yako safi. sasa umekuwa mwandishi wahabari kamili. naona interview za nguvu.
Post a Comment