Muziki wa Kiafrika unawaka moto kuliko wakati mwingine wowote ule hapa Norway. Sababu kubwa ni Ras Nas (Mnorwejiani mwenye asili ya Tanzania)
Tangu Paul Simon alipotoa albamu yake ”Graceland”mwaka 1986, mziki wa Kiafrika umekuwa ukiambukiza lahani, maudhui na ladha ya mziki wa Kimagharibi kwa kiasi kikubwa na bendi kama Coldplay, Vampire Weekend na bendi ya Kinorweji Real Ones zimekuwa zikitumbukiza na kuchanganya miondoko kadhaa kutoka Afrika Kaskazini, Afrika Magharibi na kutoka kusini mwa Afrika. Bendi za Kiafrika zimekuwa zikitumbuiza kwenye makonseti makubwa ya mziki duniani. Mziki wa KiGhana ”Highlife”, ”Afropop” wa Naijeria, Soukous kutoka Kongo na mziki wa Kiethiopia, umekuwa kwenye msamiati wa wapenzi wa mziki huku MagharibiHapa Norway kuna wanamziki maarufu wa miondoko ya mziki kutoka Afrika, wakiwemo Abuwa Adema (mwenye asili ya Naijeria), Kossa Diomande (kutoka Coté de Ivoire) na Nasibu ”Ras Nas” Mwanukuzi (Tanzania).
Konseti ya kwanza ya Ras Nas hapa Norway ilikuwa mwaka 1992, na toka wakati huko wa miaka ya 90 amekuwa akipiga mziki wake kwenye lahani ya Reggae. Ras Nas alitoa albam ya kwanza mwaka 1997 aliyoipa jina ”Cut You Loose” na albam likawa kwenye kinyang´anyiro cha ”Albam bora kuliko zote la Reggae hapa Norway”.
Albam jipya la Ras Nas liitwalo ”Dar es Salaam” ni bab´kubwa! Ina nyimbo za mchanganyiko wa miondoko ya miziki ya Kiafrika kama Soukous, Rumba na inayofanana na hiyo.
Wimbo wa kwanza ”River Nile” mzuri na mtu anaweza kusema kama umeandikwa na Linton Kwesi Johnson. Halafu unafuatia ”Guantanamo” Huu unaelezea ”Guantanamo” kama Robben Island ya wakati huu. Dar es Salaam duh! Usiseme...Halafu Zakina. Lahani ya Zakina ni ya aina yake...Hapa hata Vampire Weekend wakiiga namna gani, hawafui dafu!!!
Kwa kifupi albam ya ”Dar es Salaam” ni ya kwanza hapa Norway kupewa nyota 5 kwa mwanamziki mwenye asili ya Kiafrika. Alama ya juu kabisa ni nyota 6.

HONGERA RAS ”NASIBU MWANUKUZI” NAS!!!!
habari na Picha kwa hisani ya Nganzo Hassan Norway.
No comments:
Post a Comment