September 11, 2008

UCHUNGUZI WA CHIMBUKO LA DUNIA WAANZA

Wanasayansi wa Shirika la Ulaya linalohusika na utafiti katika masuala ya kinyuklia la CERN kwa ufupi, wamewasha mitambo yao katika majaribio ili kugunduwa vipi dunia yetu ilivyotokea. Chombo kimeanza safari zake katika eneo la majaribio hayo chini ya ardhi karibu na mji mkuu wa Usuisi, Geneva.

Mkurugenzi mkuu mteule wa Shirika la utafiti la Ulaya juu ya masuala ya kinyuklia la CERN, Rolf-Dieter Heuer anasema chombo hicho kitasaidia sana katika utafiti huo. Amesema chombo hicho kitawawezesha kuukurubia muundo wa awali wa sayari, kuukurubia mpasuko wa Big Bang na kuchipuka kwa dunia. Wanasayansi wanataraji kwa namna hiyo kupata maeleo ya kina kuhusu jinsi ulimwengu ulivyokuwa hapo awali.

Majaribio hayo ndiyo makubwa zaidi ya kisayansi ya aina hiyo kuwahi kutokea na kuwajumuisha wanasayansi karibu alfu 10 na kugharimu kitita cha dola bilioni 9 za kimarekani. 

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22