November 19, 2008

NURU NA ALI KIBA STOCKHOLM


Anaitwa Nuru Magram.Makazi yake ni ndani ya jiji la Stockholm nchini Sweden. Bila shaka unamkumbuka kwa vibao vyake kama vile Walimwengu na Msela ambavyo ndivyo vilimtoa katika ulimwengu wa muziki.
Hivi karibuni amekuwa studio akikamilisha project yake mpya ya muziki ambayo itakamilika hivi karibuni.Lakini kuonyesha jinsi ambavyo bado hajajiweka kando na mambo ya muziki, hivi karibuni mnamo tarehe 22 Novemba anatarajiwa kufungua show ya mwanamuziki mwingine wa Bongo Flava, Ali Kiba.Show hiyo itafanyikia jijini Stockholm.
Ali Kiba inasemekana ameweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kufanya tour ndefu kushinda zote zilizowahi kufanywa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya.Nuru ameahidi kufanya vitu visivyo vya kawaida hiyo tarehe 22 Novemba.Kazi kwenu wakazi wa Sweden na nchi zilizo jirani.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22