Rais mteule wa Marekani Barack Obama amekuwa na mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu kuchaguliwa, akiahidi kupambana na mzozo wa kiuchumi baada ya kuchukua madaraka Januari 20 mwakani. Obama ameongeza kuwa licha ya serikali kuwa imefanya mengi kudhibiti mporomoko wa taasisi za mikopo duniani , lakini hatua zaidi zinahitajika.
Amesema kuwa baraza la Congress linapaswa kupitisha mpango maalum wa kichocheo haraka iwezekanavyo, lakini pia ameonyesha matumaini kuwa Marekani itafanikiwa kupita katika mzozo huu.
Akizungumzia kuhusu sera za mambo ya kigeni, Obama amesema haikubaliki kwa Iran kutengeneza silaha za kinuklia na kutoa wito zichukuliwe juhudi za kimataifa kuishawishi Iran kuachana na shughuli zake nyeti za kinuklia.
No comments:
Post a Comment