November 25, 2008

Ujerumani yakataa kupunguza kodi ya mapato

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kwamba Ujerumani na Ufaransa haizotofuata mfano wa Uingereza wa kupunguza kodi ya ongezeko la thamani ya mauzo VAT.
Imeripotiwa kwamba Uingereza inapanga kupunguza kodi hiyo ya VAT kutoka asilimia 17.5 hadi kuwa asilimia 15 kabla ya X'masi kuchochea matumizi.
Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Ufaransa na Ujerumani mjini Paris Kansela Merkel amesema hatua hiyo sio jibu sahihi kwa Ufaransa na Ujerumani.
Mkutano wa mwaka huu wa mawaziri waandamizi kutoka nchi hizi mbili katika Kasri la Elysee nchini Ufaransa unatazamiwa kuja na mapendekezo madhubuti kukabiliana na mgogoro wa kifedha.Sarkozy alikuwa akitarajiwa kumshinikiza Merkel kwa mchango zaidi kwa ajili ya mpango wa kuchochea uchumi barani kote Ulaya.
Serikali ya Ujerumani tayari imejizatiti kutowa zaidi ya euro bilioni 32 kwa mpango wake wenyewe wa kuchochea uchumi.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22