December 31, 2008

MGONJWA AFARIKI CHOONI

Hufeland klinikum
Natalie F. (20)
Katika Hospital moja mjini weimar nchini Ujerumani kumetokea maajabu ambayo hata katika nchi za kiafrica au Dunia ya Tatu hayawezi kutokea, baada ya maiti ya mgonjwa kulala siku tano katika choo cha vilemabila kujulikana, inasemakana kwamba mgonjwa huyo aliaga kuwa anakwenda kutembea ikiwa ni moja ya matibabu yake, baada ya muda wake wa kurudi wodini kupita wafanyakazi na walinzi wa Hospitali walianza kumtafuta kila kona ya Hospital bila mafanikio, mpaka baada ya siku tano kupita ndio mlinzi wa Hospital hiyo akiwa katika zamu yake kuona kuwa mlango wa choo cha vilema umefungwa muda ambao kunakuwa hakuna mtu maeneo hayo ndipo alipoamua kukifungua na kukuta maiti ya mgonjwa huyo ikiwa imelala chini pembeni ya choo, pembeni yake kukiwa na chupa mbili za pombe kali moja Vodka na nyingine pombe ya kijerumani inayoitwa Doppelkorn.
Mpaka tunaenda mitamboni chanzo cha kifo hicho bado kinafanyiwa uchunguzi.

No comments: