Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya Rwanda,(ICTR), imemhukumu kifungo cha miaka 15 jela mwamuziki maarufu nchini Rwanda aliyetumia nyimbo zake kuchochea mauaji ya Watutsi nchini humo.
Mahakama hiyo iliyoko mjini Arusha nchini Tanzania imempata Simon Bikindi, mwenye umri wa miaka 54, na hatia ya kuuchochea umma kufanya mauaji ya kimbari. Mahakama ya ICTR imeeleza kuwa mwishoni mwa Juni mwaka 1994 katika tarafa ya Gisenyi, Bikindi alitangaza ujumbe kupitia spika za gari lake akiwataka Wahutu kuwaua Watutsi na baadaye alirudi tena na kuuliza endapo wametekeleza.
Mahakama imeeleza katika hukumu yake kuwa uchochezi utakaosababisha mauaji ya kimbari ni uhalifu wa hali ya juu ambao unaathiri misingi ya jamii na kutikisa hisia za kiutu.
Bikindi alikamatwa nchini Uholanzi mwaka 2001 kabla ya kupelekwa mjini Arusha kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake. Mahakama hiyo imesema adhabu yake itahusisha muda ambao tayari ameshatumia akiwa mahabusu.
Katika mauaji hayo Watutsi 800,000 waliouawa ikiwa ni pamoja na Wahutu waliochukua msimamo wa siasa za wastani.
2 comments:
kwani kaka huna picha za watu wapo uchi ukatuwekea kuangalia mana tushachoka kusoma maandishi yako mengi
Samahani Mdau, hii blog haipo kwa ajili ya picha za uchi,madhumuni yake ni kuleta habari zinazotokea duniani kote.
Karibu tena
Post a Comment