January 04, 2009

Waziri Mkuu Thuringia azinduka kutoka katika koma


Waziri Mkuu wa jimbo la Thuringia hapa Ujerumani, Dieter Althaus, anachunguzwa kuhusiana na kifo cha mtu mmoja waliyogongana naye wakati walipokuwa wakiteleza katika theluji huko Austria Alhamisi iliyopita.Taarifa ya kuchungwa kwake imekuja baada ya kiongozi kutoka chama cha Christian Democrat kupata nafuu kufuatia kuumia kichwa katika ajali hiyo ya kuteleza kwenye theluji.Waziri Mkuu wa Jimbo la Thuringia aligongana na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 41 raia wa Slovakia anayeishi Marekani ambaye alifariki wakati akipelekwa hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata.Althaus amekuwa Waziri Mkuu wa jimbo hilo la Thuringia toka mwaka 2003.

No comments: