February 23, 2009

Njia ya kuelekea Muungano wa Ujerumani

Mapinduzi ya amani, kuanguka kwa ukuta wa Berlin, kuungana tena! Makala maalum ''Nchi iliyogawika - Nchi iliyoungana'' inaonyesha njia ya kuelekea Umoja wa Ujerumani na kuonyesha vipi  njia ilivyo tangu kuugana kwa Ujerumani. Mwaka huu wa 2009 unakaribia mwaka wa ishirini tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin. Mwaka ujao wa 2010 Wajerumani watasherehekea miaka 20 ya kuungana tena kwa Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi. Tovuti ya DW-WORLD.DE itaangazia hadithi za kusisimua za Wajerumani katika sherehe za kukumbuka tukio hilo na kuhadithia juu ya hadithi jumla za kijerumani. Tutatoa maelezo kuhusu maisha ya viongozi wa mapinduzi ya amani katika Ujerumani Mashariki, DDR, kuwaruhusu walioshuhudia kuanguka kwa ukuta wa Berlin watoe ushuhuda wao na kuripoti juu ya washindi na walioshindwa katika njia ya kuelekea umoja wa Ujerumani.

No comments: