February 25, 2009

OBAMA NA MASUALA YA KIUCHUMI

MR.PRESIDENT OBAMA


Rais Barack Obama wa Marekani amekihutubia kwa mara ya kwanza kikao cha pamoja cha baraza la wawakilishi na maseneti ambapo katika hotuba hiyo aliangazia zaidi ya masuala ya uchumi na mabadiliko.

Rais Obama alisema kuwa ana matarajio mazuri ya kwamba mgogoro wa uchumi unayoikabili nchi hiyo na dunia kwa ujumla utapatiwa ufumbuzi.

Wakati ambapo akiahidi kupunguza nakisi katika bajeti ya nchi hiyo ifikapo mwaka 2013, Rais Obama alikiri ya kwamba mpango wa hivi karibuni wa kuyaokoa mabenki yanayokabiliwa na hali mbaya, utahitaji msaada zaidi kutoka serikalini kuliko ilivyofikiriwa hapo awali.

Rais huyo wa Marekani alifafanua ya kwamba mabenki ambayo yataungwa mkono na fedha za walipa kodi yatawajibika zaidi.

Akielezea  juu ya bajeti ijayo ya mwaka 2010, Rais Obama amesema Marekani haiwezi kuacha kuifanyia mabadiliko sekta ya afya na kuziangalia nchi nyingine zikichukua uongozi katika maeneo kama vile nishati endelevu.

No comments: