March 10, 2009

Jela mika sita kwa kutaka kutapeli matajiri wa kike UjerumaniMUNICH

Mtu anayetuhumiwa kwa kuwatapeli wanawake matajiri hapa Ujerumani, Helg Sgarbi amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya utapeli. 

Sgarbi ambaye ni raia wa Uswis amepatikana na makosa ya kuwatapeli matajiri wanne wa kike hapa Ujerumani na kujipatia mamilioni ya euro.

Miongoni mwao ni kujaribu kujipatia kiasi cha euro millioni 14 kutoka kwa mmiliki wa kiwanda cha magari cha BMW Susanne  Klatten, baada ya kumtishia kuwa angetoa hadharani mkanda wa video uliyorekodiwa kwa siri tajiri huyo akifanya mapenzi.

Wakili wa tapeli huyo alisoma waraka mahakamani kutoka kwa mteja wake huyo akikiri kuwa alitenda makosa hayo, hivyo kutokuwepo na haja kwa walalamikaji kufika mahakamani kuthibitisha madai yao.

1 comment:

luihamu said...

samahani fungua kurasa ya kuchangia mawazo kuhusu jumuiya ya wanablogu tanzania.

http://blogutanzania.blogspot.com/

www.ringojr.wordpress.com