March 17, 2009

KESI YA BABU WA AUSTRIA YAINGIA SIKU YA PILI

Kesi nchini Austria inayomhusu Josef Fritzl , mtu anayetuhumiwa kwa mauaji na kufanya utumwa, imeingia katika siku yake ya pili kwa ushahidi wa video unaotarajiwa kutolewa na mwanae wa kike ambaye alimfungia katika chumba kidogo chini ya ardhi kwa muda wa miaka 24, wakati huo huo akipata nae watoto saba na binti yake huyo.
Jana, Jumatatu, Fritzl alikiri kufanya makosa saba ya kujamiiana na mwanawe, kubaka na kumfungia binti yake, lakini amekana kosa la mauaji na utumwa.
Iwapo atapatikana na hatia, Fritzl, mwenye umri wa miaka 73, anakabiliwa na kifungo cha maisha.
Waendesha mashtaka wanadai kuwa alishindwa kutafuta msaada wa matibabu kwa ajili ya mtoto mchanga aliyezaliwa ambaye alikufa mwaka 1996.
Kesi hiyo inafanyika kwa faragha ili kulinda kuwatambua wahanga. Mahakama inatarajiwa kufikia uamuzi siku ya Alhamis ama Ijumaa katika mji wa Saint Polten. Kukamatwa kwa Fritzl katika mji wa Amstetten mwezi Aprili mwaka jana kulisababisha vyombo vingi vya habari kuitangaza habari hiyo.

No comments: