June 04, 2009

MISS TANZANIA-SHENGEN KUPATIKANA JUMAMOSI HII ESSEN


Shindano la kumtafuta mrembo wa tanzania katika eneo la nchi za Shengen barani Ulaya linafanyika Jumamosi hii mjini Essen nchini  Ujerumani.
Warembo wa kitanzania kutoka Norway, Holland, Ujerumani na Ufaransa wanashiriki kinyang´anyiro hicho kinachosubiriwa kwa hamu.
Mwaandaji wa shindano hilo Nashe Mvungi amethibitisha kuwa kila kitu kiko sawa, ambapo bendi ya wanamuziki wakongwe wa Afrika yenye maskani yake mjini Berlin itatumbuiza.
Katika bendi hiyo yuko mpiga solo maarufu wa zamani wa orch. Lipua Lipua, na Kamaley za Zaire ya wakati huo, Lusuama Aspro.
Pia mmoja wa wanamuziki aliyewahi kuimba na Koffi Olomide anaitwa Solei atashirikiana na kundi hilo.Soley kwa sasa anaishi  mjini Paris.
Aidha Nashe amesema kundi la wanamuziki wa kizazi kipya la kitanzania lililopo hapa Ujerumani Lizchip&Gloria litatoa burudani katika shindano hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa balozi wa tanzania nchini Ujerumani HE Ahmada Ngemera.
Katika shindano hilo, Mwenyekiti na mmiliki wa bendi za African Stars Twanga Pepeta na Vibration Sound, Baraka Msilwa atakuwa mmoja wa majaji.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22