July 02, 2009

Msichana aliyenusurika katika ajali ya ndege Comoro awasili Ufaransa.

Msichana pekee aliyenusurika katika ile ajali ya ndege katika visiwa vya Comoro amewasili nchini baada ya kusafirishwa kutoka visiwa vya Comoro. Bahia Bakari ambaye hajui kuogolea aliokolewa baada ya kuwa majini kwa zaidi ya saa 12, baada ya ndege ya shirika la ndege la Yemeni kuanguka katika bahari ya Hindi. Ndege hiyo iliyoanguka katika bahari ya Hindi siku ya Jumanne, ilikuwa imewabeba abiria 153, wengi wao wakiwa ni raia wa Comoro na Ufaransa. Bahia alisafirishwa hadi mjini Paris kwa ndege ya serikali ya Ufaransa. Babaake Kassim Bakari aliyemlaki mwanawe alisema furaha yake ilichanganyika na huzuni ya kumpoteza mkewe katika ajali hiyo.
Bado kilichosababisha ajali hiyo hakijafahamika . Wizara ya ulinzi ya Ufaransa imesema kifaa cha kurekodia mawasiliano kinachojulikana kwa umaarufu kama Black Box bado hakijapatikana licha ya ripoti za awali kusema kifaa hicho kimepatikana

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22