August 03, 2009

FISADI ARUDISHWA UJERUMANI

Mfanyabishara wa silaha ambaye ni mjerumani mwenye uraia wa Kanada,Karlheinz Schreiber amewasili nchini Ujerumani baada ya kutimuliwa kutoka Kanada.
Rufaa ya mwisho ya Schreiber alishindwa jana mjini Toronto na kuhitimisha mvutano wa kisheria uliyodumu kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Waendesha mashtaka wa Ujerumani wanatarajiwa kumfungulia mfanyabishara huyo mashtaka ya ya ukwepaji kodi, wizi na rushwa.
Mtu huyo anachukuliwa kama mhusika mkuu katika kesi inayohusiana na uepelekaji wa fedha kwa siri kwa chama cha kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl cha CDU, fedha ambazo zilitokana na mauzo ya silaha.

No comments: