Kapteni wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Togo, Emmanuel Adebayor amesema kuwa nchi yake inaweza ikajiondoa katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, baada ya basi la timu hiyo kushambuliwa na watu wenye silaha jana Ijumaa, nchini Angola. Dereva wa basi hilo aliuawa na watu tisa walijeruhiwa, wakiwemo wachezaji wawili, baada ya basi kushambuliwa wakati lilipoingia katika eneo la Cabinda.
Adebayor amesema kama usalama hautaimarishwa timu hiyo pengine inaweza ikarejea leo Jumamosi. Angola kwa upande wake imeahidi kuimarisha usalama wakati wa michuano hiyo. Akizungumza katika radio ya taifa, Waziri wa Mawasiliano ya Jamii wa Angola, Manuel Rabelais, amesema serikali ya Angola itahakikisha usalama wa kila mmoja.
Kwa mujibu wa waziri huyo, miongoni mwa watu tisa waliojeruhiwa, wanane ni raia wa Togo na mmoja ni raia wa Angola. Waziri huyo amelishutumu kundi la waasi la FLEC kwa kuhusika na shambulio hilo
No comments:
Post a Comment