Marehemu Swetu
Inaniwia vigumu sana kutoa shukran kwa mtu mmoja mmoja au kwa makundi kutokana na ushiriki wenu kuanzia kujeruhiwa mpaka mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Swetu Ramadhan Fundikira. Basi pale nitakapokuwa nimekosea kwa kumsahau kumtaja mhusika naomba radhi.
Kwa niaba ya familia ya Mzee Ramadhan Said Fundikira na ukoo wa Fundikira kwa ujumla, tunapenda kutoa shukran za dhati kwa watu wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine kwa kipindi chote cha msiba wa ndugu yetu mpendwa. Ingawa nyote mnastahili kushukuriwa lakini pia ningependa kutoa shukrani za pekee kwa uongozi na timu nzima ya Mango Garden Veteran Team kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwetu.hata mpaka baada ya mazishi,shukrani pia ziende kwenye vyombo vya habari vyote kwa ujumla yakiwemo magazeti mbalimbali,televisheni na radio zote walioshiriki katika kuupasha umma unyama aliofanyiwa ndugu yetu, naomba niishukuru sana Radio Clouds FM kwa kurusha mwenendo wote tangu mwanzo hadi mwisho wa mazishi. Madaktari na wafanyakazi wa MOI, Vituo vya Polisi cha Salender Bridge na Oyster Bay, Mkuu wa kitengo cha maabara cha Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Masheikh wa Masjid Jamia Kinondoni na kila mmoja aliyeshiriki kwa hali na mali katika mchakato mzima wa mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Swetu Ramadhan Fundikira.
Sisi wana familia hatuna cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu atawalipa Inshaallah.
Ismail R. Fundikira
Msemaji wa Familia
No comments:
Post a Comment