April 17, 2010

MAMBO YA BONGO HAYO!

Nabii Titto akinukuu neno kutoka kwenye kitabu cha mungu(BIBLIA)kinachoruhusu matumizi ya pombe huku pombe yake ikiwa pembeni

Nabii Titto akiwa katika mavazi yake ya kikazi
Mdau akisikiliza mahubiri ya Nabii Titto amesema yuko njiani kuanzisha kanisa
Hiki ndicho kipeperushi alichogawa kinachoeleza jinsi pombe inavyotibu magonjwa yote
Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahii tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara,Sikuamini maneno yake akatumwa mtu alete pombe na Nabii Titto bila hiyana kudhihirisha umma akakata safari beer,Wadau mpooo

Kipeperushi hiki cha Nabii Titto kiliwaacha wadau hoi

Juma Chikoka (Chopa mchopanga) akiwa na Jackline Wolper na Johariwakimsikiliza Nabii Titto kwa umakini mkubwa

Nabii Tito na kilaji chake

Leo nilipata mgeni wa ghafla ofisini kwangu aliyejitambulisha kwa jina laNabii Titto.Nabii Titto yeye anahubiri matumizi ya pombe kwa kutumia Biblia,anasema kuwa mungu ameruhusu watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi kwa magonjwa mbalimbali .Alikuja ofisini kwangu ili nimsaidie kurekodi kanda na cd mbalimbali zitakazomafanya watu mbalimbali duniani kupata neno lake na kunisihi sana na kuniambia nikubali kwani ilo ndio ombi mungu alilomtuma kwangu.Mimi sikumkubalia ombi lake kwani ninavyoamini mimi na imani yangu ni vitu viwili tofauti.Je Wadau mnasemaje kuhusu Nabii Titto

Picha na Maelezo kwa hisani ya Mdau wa blog hii kutoka Dar.

3 comments:

Anonymous said...

Misioni laajabu apo! kwani bombo zili anza kuuzwa ma kanisani na zili tengenezwa na ma padri!!!!

Anonymous said...

huyo jamaa kwanza ni mkatoliki na hata wakatoliki hawatangazi pombe. hakuna cha unabii ila huyo jamaa ni mlevi tuu amevaa ngozi ya punda. aende zake motoni na mipombe yake. biblia haihubiri pombe ila inahubiri mambo ya maana.

Anonymous said...

Ninavyofahamu mimi ni kwamba; hata shetani anatumia maandiko matakatifu ila ni kwa kupindisha. Mungu katika biblia anasikitika akisema: "Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa" Ni maarifa gani hayo anayosema? Ni kutolifaham neno lake linasema nini. Na hicho ndiyo kigezo anachokitumia shetani kupoteza watu wa mungu. Hawezi kuja yeye kwani watu badala ya kumsikiliza watakimbia kwa hofu ila anatummia wanadam wenzetu ambao ni mawakala wake. Huyo mtu ni upotofu mtupu hana hata hadhi ya kujiita nabii kwa mambo ayafanyayo.