April 09, 2010

WASHINDI WA NITASOMA SCHOLARSHIP PROMOTION WAJITOKEZA

Bw. Valentino J. Mhoja kutoka Dar es salaam Institute of Technology akipokea zawadi ya NITASOMA MOBILE 3 kutoka 4Layers (T) Ltd's Levis Paul akikabidhi zawadi hio Kushoto ni Bi. Venancia Donald.

Bi.Venancia Donald akipokea zawadi ya NITASOMA MOBILE 1 kwa niaba ya Witness Lucas wa Tumaini University Iringa. Akikabidhi zawadi hizo kulia ni Levis Paul Campaign & Marketing Manager 4layers (T) Ltd. Shughuli hio fupi ilifanyika leo katika ofisi ya kampuni hio iliyoko Msasani Dar es salaam.

Akielezea zaidi Bwana Levis Paul alisema promosheni hio ya NITASOMA inakuja juu kwa kasi ikiwa hii ni wiki ya tatu tangu kuanza rasmi 15.03.2010 ni matarajio yao kuchagua washindi watatu kwa vitabu vya sekondari, mwanafunzi mmoja simu ya mkononi na laptop katika wiki ya nne yaani jumatatu ijayo.


Alitoa changamoto kwa walengwa walio vyuoni na mashuleni kushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi NITASOMA UNI, au NITASOMA HIGH au NITASOMA SEC kwenda 15767 ili kushiriki katika promotion hii.
ELIMU KWANZA.

No comments: