May 04, 2010

KUCHEKA NI AFYA

Basi bwana.....

Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi kati yao ......

Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi alomfanyia mkewe ili wapime nani kubobea zaidi kwenye hiyo fani.

Mbishi 1
akasema:
Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia mke wangu simu usiku kafungua simu hakusema
haloo...kulaleki! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.


Mbishi 2
akatia:
Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lkn hakusema karibu mume wangu...aliniangalia tu...nikaona analeta
madharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.

Mbishi 3
akaunganisha:
Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu
tulipooana alikuwa anaona haya kunigusa... ananidengulia eti! na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

Mbishi
1 na 2:
Aaaaaaaah faza! acha usanii, nyie si mna watoto wawili lakini?

Mbishi
3:
Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi...
kwani mi nataka mchezo, ala!.

No comments: