June 28, 2010

UJERUMANI YATINGA NANE BORA

Wachezaji wa ujerumani wakishangilia goli la 4
Kipa wa Ujerumani akiangalia shuti la lampard likiingia wavuni

Ujerumani imeichabanga Uingereza mabao 4-1 na kuingia robofainali ya kombe la dunia kwa kishindo kikubwa.Uingereza ilikataliwa bao lake la kusawazisha, la mkwaju wa Frank Lampard, lakini hata hivyo ilishindwa kabisa kuzuia kasi ya wachezaji wa Ujerumani.

Mabao ya Ujerumani yaliwekwa wavuni na Miroslav Klose, Lukas Podolski na Thomas Müller aliyepachika mawili.

Katika mechi hiyo iliyokuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa na washabiki kote duniani, mshambuliaji wa Bayern Münich Thomas Müller alichaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mechi.

Ujerumani sasa itapambana na Argentina siku ya jumamosi

No comments: