July 30, 2010

Mahojiano ! moto ! moto kati ya Ras Makunja na Radio Free Africa Mwanza

Ras Makunja kamanda wa Ngoma Africa Band!


Mahojiano ! moto ! moto
Radio Free Africa ya mwanza ! na Ras Makunja kamanda wa Ngoma Africa Band!
Radio Free Africa ya Mwanza ! Yawaletea mahojiano maalumu
Na Ras makunja kamanda wa Ngoma Africa Band siku ya
Jumamosi 31-07-2010 saa 4 hasubui
Habari za uhakika zinaeleza kuwa kituo cha Redio Free Africa kinachorusha
matangazo yake mjini Mwanza,kitafanya mahojiano na Mwanamziki mashuhuri
Ebrahim Makunja alimaarufu kama Ras Makunja kamanda wa ffu! wa bendi
maarufu barani ulaya "The Ngoma Africa Band" yenye makao yake Ujerumani.
Mahojiano hayo yataanza saa 4 hasubui siku ya jumamosi 31-07-2010 katika
kipindi maalumu ambacho mtangazaji wa redio hiyo Prince Baina Kamukulu
ataongoza timu ya kumlima maswali Ras Makunja,mwanamziki ambaye ametajwa
mara nyingi na vyombo vya habari vya ndani na nje nchi kuwa ni mtunzi mwenye
hoja nzito kwa jamii,mara nyingine nyimbo zake utoa cheche za moto na kuwafanya
walengwa wanao perekewa ujumbe wasipate usingizi!
Radio hiyo itamrusha hewani Live Ras Makunja, ambae ndie mpishi wa nyimbo nyingi
ikiwemo CD yao mpya "Jakaya Kikwete 2010" CD ambayo imeshaingia nchini
na inaweza kutingisha anga wakati wowote!
Wasilizaji zaidi ya milioni 200 wa afrika mashariki na kati wanatarajiwa kusikiliza mahojiano
hayo ya Radio Free Africa na Ras Makunja,mahojiano ambayo yanatabiliwa kuwa yatakuwa
ya "Jino kwa Jino" au "Jicho kwa Jicho"
wewe msikilizaji usikose kuyanasa mahojiano hayo kambambe

1 comment:

Anonymous said...

Kamanda mkuu wa ffu,kaka mkubwa wa watoto wa mbwa najua lazima utabwaka sana pale