September 11, 2010

Aliyetoa matamshi ya kibaguzi Ujerumani ajiuzulu

Thilo Sarrazin

Mwanachama wa bodi ya uongozi ya Benki ya Ujerumani, Thilo Sarrazin, amekubali kujiuzulu kufuatia matamshi yake dhidi ya wahamiaji wa Kiislamu nchini Ujerumani.

Amesema atajiuzulu kutoka katika nafasi yake hiyo ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Sarrazin alizua mtafaruku baada ya kutoa kitabu chake ambapo alisema kuwa wahamiaji wa Kiislamu nchini Ujerumani wameshindwa kujishirikisha na jamii ya Wajerumani na kwamba wayahudi nao pia wana tabia kama hiyo.

Chama cha Social Democrats, ambacho Sarrazin ni mwanachama wake, kinadhamiria kumfukuza uanachama, lakini ameungwa mkono zaidi kutoka baadhi ya wanachama wa ngazi ya juu na wakawaida wa chama hicho.

chanzo.DW-Bonn

No comments: