September 04, 2010

friends connects

Kwanza pole na kazi zako zote za kila siku na asante kuendelea kutupa burudani taarifa za papo kwa hapo kila wakati tunapo hitaji, umetufikia mpaka huku machimboni.


TOVUTI MPYA YA FRIENDS CONNECT ZONE

Nilikua naomba unisaidie kunitambulishia tovuti yangu ambayo ni mpya kabisa machoni kwa watu wote mimi ni mtanzania. Baada ya kukaa chini na kufikiria nimeona nije na wazo jipya la kuanzisha tovuti ambayo itawakutanisha watanzania mbali mbali na watu mbali mbali popote Duniani, kwa lugha ya kigeni tunaita Social Network.

Katika tovuti hii ya Friends Connect Zone. ni rahisi sana kutumia na pia kujiunga, pia mtumiaji anaweza jiunga kupitia Facebook ama myspace mtumiaji akiwa ndani ya tovuti hii ataweza tafuta marafiki,ataweza weka picha zake,video,blogs na mambo mengine mengi.


Si hivyo tuu mtandao huu mpya utakuwezeshaƔkuchat muda wote ambao atakuwa hewani na marafiki watakao kuwa hewani,pia ataweza kuona yuko wapi katika muda wa nchi aliyopo.


Nawaombeni ndugu zangu tujiunge katika mtandao huu, na pia tuwaalike na wenzetu wapate kujiunga, kwa pamoja tuendeleze tecknolojia nchini kwetu,na mawasiliano kwa ujumla, nawashukuruni nyote na karibuni sana.

Jina la website: Friends Connect Zone


Link ni: http://www.friendsconnectzone.tk/


email:friendsconnectszone@gmail.com


Natanguliza shukurani zangu....pamoja tunaendeleza Burudani na Habari Ndani ya Malumbo Junior web blog.

No comments: