December 12, 2011

Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika yatingisha jiji la Berlin.‏

BOSCO,EMANUEL,SUDI
Mh. Balozi Ngemera Akitoa Hotuba katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, kulia Naibu balozi Mh. Siwa na Mzee Temu
Mh. Balozi Ngemera Akitoa Hotuba katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru

MDUARA
MZEE TEMU, MIMI NA MH.NAIBU BALOZI SIWA
F.F.U WAKITEMBEZA VIRUNGU
NYOMI

Mamia za Watanzania kutoka katika pande tofauti nchini Ujerumani, walikusanyika jijini Berlin, kwa lengo la kufurahi pamoja kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania Bara.

Hafla hiyo iliyofanyika kwa namna tatu tofauti, ilianza kwa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania Ijumaa, ikiwa siku ya kilele, siku hiyo ilibatizwa jina la usiku wa kidiplomasia ambapo mabalozi wa Afrika nchini Ujerumani walijivinjari katika sherehe ya jioni iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Hafla hiyo ya kidemokrasi ilivunja hata protokali ya aina hiyo ya watu pale ambapo walijikuta katika kizimba cha burudani wakisakata rhumba lililokuwa likiporomoshwa na Ngoma Afrika Bend AKA F.F.U chini ya usimamizi wa kamanda Ras Makunja.

Jumamosi mchana ikiwa siku za mdahalo ambapo washiriki walijadili kwa kina namna ya kusaidia wenzao huko nyumbani, si kisiasa bali kwa vitendo katika nyanja mbalimbali za maendelea zikiwemo za kielimu na kiafya.

Kama vile haitoshi, usiku wa kuamkia jumapili watoto wa mitaa ya Berlin,Augsburg, Bonn, Munich, Cologne, Essen, Frankfurt na kwengineko walisema watajiachia siku za jumamosi, pale ambapo pamoja na Ngoma Afrika kurusha walimwengu hao Taarab, Bongo, Flava na muziki mwingine ulipata nafasi.
Pia alikuwepo mwanamuziki mkongwe Afrika mashariki ambaye makazi yake kwa sasa ni hapa ujerumani Tabia Mwanjelwa alikonga nyoyo za mashabiki kwa muziki wa dansi.
Hakika Ulaya wacha iitwe ulaya watu walipendeza, ni usiku wa baridi lakini viguo vilivaliwa kina kaka na kina dada, kina mama na watoto ili mradi tu kila mtu alikonga moyo wake.

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22