June 15, 2012

KAULI YA KWANZA YA DOGO JANJA BAADA YA KURUDISHWA KWAO NA MADEE.

Kama ulipitwa na hii stori ni kwamba msanii Madee wa TipTop Connection ambae ndio alikabidhiwa kumlea Dogo Janja na kumsimamia kwenye muziki alitangaza juzi kwamba amemrudisha Dogo Janja kwenye mikono ya wazazi wake baada ya kuona muelekeo wa Janja sio mzuri kitabia.Alisema kwanza Janja alikua mtoro wa shule na mara kadhaa hakwenda shule na alikua akimdanganya, aliwahi kumkuta anaogoelea Ubungo Plaza wakati wenzake wako shule, amekuta msg za matusi ambazo Dogo Janja aliwatumia watu wengine kuhusu Madee na makosa mengine kadhaa.Dogo Janja ambae sasa hivi karudi Arusha tayari amefunguka kila kitu katika Interview ya Dakika 40 Exclusive on millardayo.com na yafuatayo hapo chini ni baadhi ya mambo aliyoyazungumza.Amesema “kwanza napenda watanzania wajue kwamba mimi nilikua siishi na Madee nilikua naishi na rafiki yake ambae ni Abdallah Doka Kimara jirani na Madee, Madee alikua haniangalii kwa chochote na niliweka kikao juzi kati tu hapa nilikua nataka nirudi kwetu, kula ni Doka, kuvaa Doka, Hela ya Shule Doka…. ninavyoongea hapa Dogo Janja sijawahi kulipwa hela zaidi ya laki tatu kwenye show, Tanzania hii nimeshaizunguka ujue alafu sioni faida yake nakwenda kwenye show nikirudi napewa laki moja alafu ukiuliza mtu anaweza kukununia sasa nikawa zinanikera lakini nikawa nashindwa kuongea sababu ndio niko pale kwa ajili ninasoma

”KUHUSU ACCOUNT YANGU BANK:

Madee alininyang’anya mpaka kadi yangu ya ATM yani mimi narudi Arusha ni kama nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme labda narudi Arusha ni kama vile nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme labda naweza kurudi Arusha labda kwenye account sijui nina shilingi ngapi, kachukua hela zangu zote kwenye account yani, mi nilikua namuona mwema ananijali aliniambia nenda kafungue account na kiuaminifu pale unatakiwa kuandia namba zako mimi sikuandika zangu nikaandika za Madee, taarifa yoyote ya bank inakutana na Madee, mi siwezi kumtusi yule nitakua namkosea sana hata akinipa radhi inaweza kunipata mi naongea kilicho moyoni mwangu mpaka nimechukua hatua hii

KURUDISHWA KWANGU ADA SHULENI NA KIWANGO CHA PESA BANK:

Na jina lote hili Dogo Janja nilikua narudishwa ada nyumbani, nikachukua hatua nikaenda kufanya show ile hela yangu ya show baada ya kurudi nakumbuka alitoa laki mbili na 60, hela ilikua yangu akaniambia… Ahh Janja hapa sina hela nyingine nenda katoe kwenye account nitakurudishia.. ni brother alafu mi namuheshimu sana, kadi yangu ya bank yeye ndio alikua anaizuia lakini mwisho wa siku nakuja kuangalia account yangu, mbona account haisomi? na kadi yangu yeye ndio alikua nayo… Millard nakwambia ukweli wa mwenyenzi Mungu mimi account yangu haikuwahi kufikisha shilingi milioni moja na kila show ninayofanya nalipwa shilingi milioni moja, naongea mbele za mwenyenzi Mungu mimi mtoto wa kiislamu naitwa Abdulaziz

”KUHUSU SHOW YA MWISHO KUIFANYA KABLA YA YEYE KUNIPIGA:

Madee alinipigia simu jumapili akiwa Iringa ambapo jumanne wenzangu walikua wanaanza mtihani,nilimwambia niko na Hassan nyumbani kwa Tunda akasema ana kaka yake Kibaha alikua na show ya CCM alikua anamtaka lakini akaona hawezi na analove na bro akashindwa kukataa, roho ilikua inaniuma mimi hapa mimi nakwenda kufanya show kwa laki moja… alafu hapo niko na backup wangu nimempa elfu 20 mi nikabaki na elfu 80 alafu hiyo 80 anakupigia…. wee sikia elfu 50 hiyo kaweke bank, elfu 50 tumia…. mi nikafanya kipeace tu nikaenda kwenye show huyo brother wake kachelewa kuturudisha hapa saa saba usiku kwa sababu ujue mimi sina usafiri na yule jamaa alikua anasubiri mishe zake zote zikamilike alafu asubuhi nilikua natakiwa kuingia shule, kosa sio langu ni la huyo kaka yake Madee.. sikwenda shule jumatatu sababu nilichelewa.. hivi hata wewe Millard unaweza kulala saa saba ukaamka saa kumi??????! hiyo siku ndio nilitakiwa kwenda kuchukua namba ya mtihani nikapangwe la dawati langu ili jumanne nifanye mtihani, nilipoona nimechoka nilimpigia mwalimu wa Darasa nikamwambia siwezi kwenda shule jumatatu akaniambia hamna neno mi nikienda jumanne siku ya mtihani niende asubuhi nitapata

”JINSI MADEE ALIVYONIPIGA:

Nilikua nyumbani kwa Tunda Man na Hassan ambae aliniacha baada ya kutumwa, nimekaa kidogo natoka hivi nakutana na Madee geitinihajaniuliza chochote zaidi ya kuanza kunipig, kanichezeshea mikono kanipiga makofi alafu kanidhalilisha yani mtaa mzima umekusanyana pale kwa Tunda Man, t shirt ilichanika na akanikatalia kupanda kwenye gari… roho iliniuma palepale alafu alivyonikatalia kupanda kwenye gari huku akiniambia anikute nyumbani baada ya dakika tano, roho iliniuma nikasema haya yote nayapata kwa sababu mimi ndio nataka na napenda muziki na napenda baadae niwe na maisha bora, niliongea na wazazi wakaniambia nivumilie lakini kiukweli nikasema siwezi tena kuishi Dar es salaam na leo June 13 2012 ndio siku ya mwisho kuishi Dar es salaam hapa ninavyoongea, jioni niliitisha kikao nikampigia Doka, Madee, na kaka yangu huyu nikaulizwa labda kuna kitu Madee hanifanyii mi nikashindwa kuongea nikasema bwana mimi sitaki chochote mi nirudisheni kwetu ujue Millard mpaka mimi nachukua maamuzi haya kwamba naomba nirudishwe kwetu, nimeomba nirudi kiroho safi tu lakini nashangaa yeye anapokwenda kuongea mambo mengine kwenye media, mi namshangaa yule ni mtu mzima anajielewa ujue, sasa mimi sijui kwa nini amekua hivyo

”KUHUSU MADEE KUMUOMBA BABA YANGU ANIAMBIE NISIONGEE CHOCHOTE KWENYE MEDIA:

“Alimpigia simu baba ya kumuomba nisizungumze chochote kwenye media akidai kwamba itakua aibu kwangu na kwake, mimi niko hewani lakini hakunipigia.. baadae nikapata simu kutoka kwa bro akaniambia niongee na mama nilipoongea nae akaniambia Madee kasema nisiseme chochote kwenye radio, sasa imefika jioni nikashangaa nikamsikia sasa nikajiuliza kwa nini kaongea? na mimi siwezi kumpigia yule simu yani nimeshaapia kwa mwenyeenzi Mungu siwezi kumpigia simu.KUHUSU MIMI KUACHA MUZIKI: “Roho inaniuma kichizi nimeona hiviii, yani huu mziki huu kwa sababu haunisaidii chochote, mimi narudi Arusha ni kama narudi tena kuanza maisha mapya kwa hiyo mimi nimeona bora tu kama inawezekana huu muziki naweza kuacha na nitaishi kama zamani kwa sababu kwetu sijaua, nimeona bora nitulie nyumbani ujue mpaka Millard pale nimeomba kabisa jamani Eeehe nirudisheni nyumbani kwetu, nasema Inshallaah mwenyeenzi Mungu yupo na mimi na riziki hapangi Madee riziki anapanga Mungu”

KUHUSU KUSOMA DAR ES SALAAM:

“Sitaki kabisa kusoma Dar es salaam mimi nakwenda kusoma Arusha au mkoa wowote sitaki tena.

Chanzo:Millard Ayo.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22