July 16, 2012

UJUMBE WA AFANDE SELE KWA 20PA

AFANDE SELE

Uswahiba kati ya wasanii wawili wa Bongo Flava nchini, Afande Sele na 20 Percent umeingia dosari baada ya kutupiana maneno kila mmoja kwa nyakati tofauti kwenye vyombo vya habari.
Maneno hayo yalianza wiki iliyopita baada ya Afande Sele kuzungumza na Clouds FM na kudai kusikitishwa na kitendo cha swahiba wake 20 Percent cha kugoma kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za Zanzibar wakati alikuwa amelipwa pesa zote.
Kufuatia mgomo huo, waandaaji walimpeleka lock-up msanii huyo na kubaki na laptop yake mpaka pale atakapowarudishia waandaji hao shilingi milioni moja waliyompa kwa ajili ya kuperform kwenye tuzo hizo.
Hatimaye jana 20 Percent alizungumza na kituo hicho cha radio kuhusiana na tukio lenyewe na kusema kuwa Afande Sele amechanganyikiwa na anasumbuliwa na njaa ndio maana anamlaumu.
Akiongea kwa jaziba, 20 Percent amesema Afande Sele ni kama ‘mtoto’ na alimshangaa kufahamu kuwa alifika Zanzibar saa sita usiku bila kujuwa sehemu ya kulala kutokana na waandaaji hao kuwa wababaishaji.
Juzi kati kupitia ukurasa waFacebook Afande Sele alicaharanga walaka ufuatao:
“Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twenty Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma "MBELE YAKO NYUMA YANGU" .. Kuna mstari Nilisema " ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugumu, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu".
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mmefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22