June 25, 2013

MAPAMBANO YA VUNJA JUNGU

kuna pambano la ngumi la aina yake katika historia ya ngumi ambalo
litapigwa siku ya tarehe 30/6/2013 ambayo ni wiki ya mwisho kabla ya
kuingia mwezi wa ramadhan,ambapo waumini wa dini ya kiislam hufunga na
shughuli nyingi za starehe ,michezo na anasa nyingine hupungua ndani ya
mwezi huo, hivyo ni wiki la vunja jungu ndio pambano la mabondia wakatili
ulingoni na wapole nje ya ulingo na wacha mungu sana YOHANA ROBERT NA
YOHANA MATHAYO watazipiga katika ukumbi wa friends corner hotel pale
manzese. ni pambano lenye upinzani mkali kutokana na sifa za mabondia
wenyewe kutokuwa na mzaha wawapo ulingoni na ni mabondia wasiokubali
kushindwa, hiyo nayo ni sifa mojawapo inayowafanya wawe na rekodi
nzuri katika ngumi za kulipwa hapa nchini.
akilizungumzia pambano hilo Ibrahim kamwe kwa niaba ya muandaaji mkuu
mwalim hatibu anasema kuwa maandalizi yamekwenda vizuri na mpaka sasa
hakuna tatizo lolote kwa mabondia hao watakaocheza pambano kuu wala wale wa
utangulizi ambao ni   Fabian lyimo  atazipiga na musa sunga pambano la
raund nane huku Bakari ustadh atazipiga na frank zagarino, wakati huohuo
Tasha mjuaji na Rama johncena watatoana jasho. Pia Yule bingwa wa PST uzito
mdogo (minimum weight) goldsilver ataumana vikali na bondia kutoka klabu ya
bigright boxing herman Richard. Nae Ibrahim kamwe anaongeza kwa
kusema hilo, linaweza kuwa pambano kali sana la vunja jungu ambalo
halijawahi kutokea kutokana na sifa na mabondia wenyewe na jinsi walivyo
kamiana na uwezo mzuri wa kutupa makonde walionao

No comments: