January 04, 2014

Mazungumzo ya amani Sudan Kusini bado kitendawili

Wapatanishi wamesema kuwa sasa haijulikani wazi kama waasi wa Sudan Kusini wataanzisha mazungumzo ya ana kwa ana na serikali, hali ambayo imeondoa matumaini ya kusitishwa mapigano mara moja ili kuiepusha nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. 
Mazungumzo yaliyopangwa katika nchi jirani ya Ethiopia,  tayari yamecheleweshwa mara kadhaa, pamoja na kuwa na mwanzo mbaya. Pande zote mbili walikutana na wapatanishi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi IGAD kwa siku ya pili hii leo lakini hawakukaa katika meza moja.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Ethiopia Dina Mufti amesema bado wanaendelea kutayarisha agenda kuu  ya mazungumzo hayo ambayo itakubaliwa na pande zote.  
Mapigano yalizuka mwezi uliopita katika nchi hiyo changa kabisa ulimwenguni, baada ya Rais Salva Kiir  kumtuhumu aliyekuwa naibu wake kwa kupanga jaribio la mapinduzi ambalo halikufaulu. 
Maelfu wanahofiwa kuuwawa na wengine 200,000 wameyakimbia makaazi yao.

Chanzo. Dw.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22